Jina la Usajili:  Neno la Siri:    Umesahau neno la siri?   |   Umesahau jina?
12 Machi 2011

Wasanii sio 'Mzuka Kuzimwaga' Tuzo

Wasanii

UMAKINI katika mpangilio mzima wa utoaji wa Tuzo za Kili Music zinazoratibiwa na Baraza la Sanaa la Taifa nchini (BASATA), unatakiwa uwe na mpangilio na elimu ya kutosha itolewe kwa washiriki.

Maoni ya Tanzania Daima leo yamefuatia wingu la wasanii ama vikundi mbalimbali kutangaza kujitoa huku kila mmoja au kikundi ama bendi ikitoa sababu moja tu ya kutoridhika na mpangilio mzima wa utoaji wa tuzo hizo ambazo zinashika nafasi ya pili barani Afrika, zikitanguliwa na KORA Music za Afrika Kusini.

Sisi wadau wa tasnia hii ya muziki tunaamini jambo hili kwanza linadhihirisha jinsi wasanii, bendi na makundi wasivyojiamini katika ushindani.

Awali ya yote, wanapaswa kutambua kwamba kuwepo kwao katika orodha ya washiriki ni washindi tayari, lakini kujitoa inaonyesha jinsi wasivyo na nidhamu katika kazi zao na kutojiamini kwa ujumla.

Kadhalika upo usemi kwamba asiyekubali kushindwa si mshindani na hivi ndivyo inavyodhihirika.

Kama wewe ni msanii unayejiamini na kazi yako ni bora, kwa nini ujitoe? Kujitoa kwenu ni njia moja au nyingine ya kuwanyong’onyeza na kuwanyima haki yao ya msingi mashabiki wenu.

Mpaka jana wasanii kadhaa wameendelea kutangaza kujitoa katika mchakato unaoendelea wa utoaji wa tuzo za muziki ambazo hufanyika kila mwaka.

Waliotangaza kujitoa kutokana na kutoridhishwa na mpangilio ni bendi ya FM Academia, ambapo itakuwa bendi ya pili kutangaza kujitoa, ikiwa imetanguliwa na bendi ya Kalunde, ambao walijitoa mapema.

Katika hili, bendi hizi zitakuwa zimejiondoa, huku wakisahau kwamba walikwisha kuwahi kushiriki katika miaka ya nyuma na wote walipata tuzo.

Hivyo, kwa kutoa sababu kwamba mpangilio haukuwa mzuri kwa mwaka huu, inashangaza, kwani waliposhinda katika miaka ya nyuma mpangilio ulikuwaje?

Jambo la muhimu ni kutoa kazi zenye ubora wa hali ya juu, ambazo zitaleta ushindani madhubuti katika muziki, kwani kujitoa si suluhisho.

Login to post comments

MSANII WA WIKI

Loveness

MUIGIZAJI na Mtayarishaji wa Filamu Tanzania Loveness Watson Nyota yake kwa sasa inatingisha katika tasnia ya

Soma Zaidi...

VIDEO YA MHARIRI

Off Side

Si mara ya kwanza kutazama filamu za Kanumba, lakini pia ni ukweli kwamba kila filamu anayokuja nayo

Soma Zaidi...

FILAMU ZA BONGO

Mbawa za Dino Zafunguka

MUIGIZAJI na Mtayarishaji wa filamu hapa nchini Tanzania Dennis Sweya (Dino) anatarajia kuanza kurekodi

Soma Zaidi...

WAHAPAHAPA VIDEO

You need Flash player 6+ and JavaScript enabled to view this video.