Jina la Usajili:  Neno la Siri:    Umesahau neno la siri?   |   Umesahau jina?
25 Machi 2011

Wabunge Ndani ya Tamasha la Uzalendo

Wabunge Ndani ya Tamasha la Uzalendo

Wabunge katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, viongozi wa vyama vya siasa na asasi za kiraia, watahudhuria tamasha kubwa la kuhamasisha uzalendo nchini, linalotarajiwa kufanyika Machi 26, 2011 kwenye Viwanja vya Biafra, Kinondoni, Dar es Salaam.

Tamasha hilo linaloandaliwa na Kampuni ya Global Publishers & General Enterprises Ltd kwa

kushirikiana na Clouds Media Group, litashirikisha pia watoa mada kutoka kada mbalimbali na wasanii wa fani karibu zote likiwa na kauli mbiu "TAMASHA LA UZALENDO: TANZANIA KWANZA, SISI SOTE NI NDUGU."

Mratibu wa tamasha hilo, Juma Mbizo kupitia taarifa yake kwa vyombo vya habari jana, alisema kuwa wabunge hao, viongozi wa kisiasa na wale wa asasi za kiraia, wamekubali mwaliko wa kufika kusikiliza mada zitakazotolewa zenye dhumuni la kuwatuliza wananchi na kuipenda nchi yao.

"Wabunge kama ilivyo viongozi wa kisiasa ni wawakilishi wa wananchi, kwa hiyo ni busara kuona wamekubali kufika kusikiliza kitakachozungumzwa," alisema Mbizo na kuongeza: "Tamasha ni la wazi na bure, hivyo kila mtu afike. Litaanza saa 5:00 asubuhi na kufika mwisho saa 12:30 jioni."

"Tunawahimiza Watanzania waje kwa wingi kusikiliza ujumbe utakaolewa. Kutakuwa na wasanii wakubwa wa Bongo Fleva, Reggae, nyimbo za Injili, bendi za muziki wa dansi. Vilevile kutakuwa na burudani za sarakasi na maigizo yenye ujumbe wa kuhamasisha uzalendo," alisema Mbizo.

 

Login to post comments

MSANII WA WIKI

Loveness

MUIGIZAJI na Mtayarishaji wa Filamu Tanzania Loveness Watson Nyota yake kwa sasa inatingisha katika tasnia ya

Soma Zaidi...

VIDEO YA MHARIRI

Off Side

Si mara ya kwanza kutazama filamu za Kanumba, lakini pia ni ukweli kwamba kila filamu anayokuja nayo

Soma Zaidi...

FILAMU ZA BONGO

Mbawa za Dino Zafunguka

MUIGIZAJI na Mtayarishaji wa filamu hapa nchini Tanzania Dennis Sweya (Dino) anatarajia kuanza kurekodi

Soma Zaidi...

WAHAPAHAPA VIDEO

You need Flash player 6+ and JavaScript enabled to view this video.