Jina la Usajili:  Neno la Siri:    Umesahau neno la siri?   |   Umesahau jina?
28 Machi 2011

Tamasha la Pasaka, Shusho Ndani

Shusho

MUIMBAJI wa muziki wa Injili mwenye kipaji cha aina yake awapo jukwaani, Christina Shusho, naye amethibitisha kushiriki katika tamasha kubwa la Pasaka litakalofanyika siku ya sikuu ya Pasaka Aprili 24 katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama, ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Msama Promotions ya jijini Dar es Salaam, alisema Shusho anakuwa ni mwimbaji wa nane kuthibitisha.

“Shusho tutakuwa naye kwenye tamasha siku hiyo na kutumbuiza mbele ya mgeni rasmi Rais Jakaya Kikwete, na naamini mwaka huu tamasha hili litakuwa bora zaidi kutokana na kushirikisha waimbaji wengi wakali,” alisema Msama.

Tamasha la Pasaka la mwaka huu litakuwa la aina yake chini ya mgeni rasmi Rais Jakaya Kikwete huku likishirikisha waimbaji mahiri kutoka ndani na nje ya Tanzania.

Msama alisema tamasha hilo baada ya kufanyika jijini Dar es Salaam, pia litarindima kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma Aprili 25.

Alisema, baada ya hapo itakuwa zamu ya wakati za Kanda ya Ziwa pale litakapofanyika kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza Aprili 26, Sikukuu ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Alisema malengo ya tamasha la mwaka huu, ni kuchangisha fedha kwa ajili ya kuwasomesha watoto yatima na kuwasaidia mitaji wanawake wajane.

Zaidi ya hapo, fedha nyingine zitatumika kwa ajili ya kuwasaidia waathirika wa mabomu yaliyotokea kambi ya JWTZ Gongo la Mboto jijini Dar es Salaam, tukio lililotokea Februari 16.

Shusho miongoni mwa waimbaji mahiri wa nyimbo za injili nchini, siku hiyo atashirikiana na waimbaji wengine kama Upendo Nkone, Rose Muhando, Boniface Mwaitege.

Wengine ni Annastazia Mukabwa, Pamela Wanderwa na Solomon Mukubwa kutoka Kenya ambao wote tayari wamethibitisha na Ephraem Sekeleti kutoka Zambia.

Kiingilio katika tamasha hilo kitakuwa sh 4,000 kwa viti maalum B ni sh 10,000 na maalum A sh 20,000, tiketi za kategoria hiyo hazitauzwa mlangoni.

Wakati tiketi za viti maalum VIP A zitakuwa kama meza za familia.

1 maoni

  • Maoni jeni 01 Mei 2011 jeni

    wahapahapa unafanya kazi nzuri sana ubarikiwe mimi ni shabiki wa glob yako haipiti siku sijakutembelea napenda blog yako sana kitu nilikuwanakuomba utuwekee player ya nyimbo za dini haswa ya bonny mwaitege wimbo wake mpya njoo ufanyiwe maombi na christina shusho kama atakuwa na wimbo mpya tafadhali utuwekee ni hayo tu otherwise unafanya vizuri

Login to post comments

MSANII WA WIKI

Loveness

MUIGIZAJI na Mtayarishaji wa Filamu Tanzania Loveness Watson Nyota yake kwa sasa inatingisha katika tasnia ya

Soma Zaidi...

VIDEO YA MHARIRI

Off Side

Si mara ya kwanza kutazama filamu za Kanumba, lakini pia ni ukweli kwamba kila filamu anayokuja nayo

Soma Zaidi...

FILAMU ZA BONGO

Mbawa za Dino Zafunguka

MUIGIZAJI na Mtayarishaji wa filamu hapa nchini Tanzania Dennis Sweya (Dino) anatarajia kuanza kurekodi

Soma Zaidi...

WAHAPAHAPA VIDEO

You need Flash player 6+ and JavaScript enabled to view this video.