Jina la Usajili:  Neno la Siri:    Umesahau neno la siri?   |   Umesahau jina?
29 Machi 2011

Rich One na Mikakati ya Albamu

rich_one

MSANII mahiri wa muziki wa kizazi kipya Richard Shauri ‘Rich One’, amesema pamoja na kuwa kimya lakini anaendelea na kazi zake ambapo hivi sasa anapiga mahesabu ya kutafuta kipindi muafaka cha kuiingiza sokoni albamu yake mpya anayoiandaa.

Rich One mmoja wa wasanii waliojitoa kutoka TMK Wanaume Halisi na kuanzisha kundi ambalo limeshindwa kusimama la Wanaume, alisema, ametengeneza nyimbo kadhaa za albamu hiyo binafsi, ingawa kuna wasanii aliowashirikisha katika baadhi ya nyimbo.

Hata hivyo alisema kuwa, tangu kutokea kwa maafa yaliyotokana na mlipuko wa mabomu ya Gongo la Mboto, ambayo yalisababisha baadhi ya wananchi kupoteza maisha na mali kutekea, hajafanya kazi.

“Kaka pamoja na kuwa nipo kimya lakini naendelea na kazi kimya kimya, kwa sasa nimekaribia kukamilisha albamu yangu binafsi, nimeamua kutoitangaza kwanza kwa sababu ninachunguza kujua muda muafaka wa kuiingiza sokoni,” alisema Rich One.

Aidha alisema atakuwa miongoni mwa wachezaji wa timu ya wasanii wa Bongo Fleva itakayosafiri mapema mwezi ujao kwenda jijini Mwanza kucheza mechi maalum na waandishi wa habari wa mkoa huo, kwa ajili ya kuchangia maafa ya Gongo la Mboto.

Hivi karibuni timu hiyo ilicheza mechi ya kirafiki na wasanii wa filamu nchini na kuishindilia mabao 2-0 katika mechi ya kuchangia waathirika wa mabomu ya Gongo la Mboto, iliyopigwa kwenye dimba la taifa jijini Dar es Salaam.

na Ruhazi Ruhazi

Login to post comments

MSANII WA WIKI

Loveness

MUIGIZAJI na Mtayarishaji wa Filamu Tanzania Loveness Watson Nyota yake kwa sasa inatingisha katika tasnia ya

Soma Zaidi...

VIDEO YA MHARIRI

Off Side

Si mara ya kwanza kutazama filamu za Kanumba, lakini pia ni ukweli kwamba kila filamu anayokuja nayo

Soma Zaidi...

FILAMU ZA BONGO

Mbawa za Dino Zafunguka

MUIGIZAJI na Mtayarishaji wa filamu hapa nchini Tanzania Dennis Sweya (Dino) anatarajia kuanza kurekodi

Soma Zaidi...

WAHAPAHAPA VIDEO

You need Flash player 6+ and JavaScript enabled to view this video.