Jina la Usajili:  Neno la Siri:    Umesahau neno la siri?   |   Umesahau jina?
30 Machi 2011

Kauli ya JK Yakanganya Wasanii

kikwete

Huku Rais Jakaya Kikwete akitoa tamko la kuwajibu wasanii wa muziki wa kizazi kipya nchini na kuwataka waache malumbano kuhusu umiliki wa studio na kusisitiza kuwa ametoa vifaa hivyo kwa wale waliomwomba, suala hilo limezua utata zaidi.

Tofauti na hotuba yake ya wakati akizindua Bunge la 10 mjini Dodoma mwaka jana ambako Rais Kikwete alisema amesikia kilio cha wasanii na kuamua kuwapa studio, tamko lake la sasa linapingana na mtazamo wake wa awali.

Wiki iliyopita, akizungumza kwa niaba ya mkuu wa nchi katika Jukwaa la Sanaa lililofanyika Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) jana Mkurugenzi wa Idara ya Utamaduni wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Angela Ngowi alisema rais ametoa tamko hilo kwa maandishi, hivyo ni wajibu wa kila msanii kulielewa.

Ngowi alinukuu kauli hiyo fupi ya Kikwete isemayo, "Nimetoa vifaa vya mastering studio kwa ajili ya wasanii walioomba kwangu kupitia risala, hata hivyo wasanii wote wanaruhusiwa kuitumia na ikiwa kuna yeyote anahitaji anapaswa kuleta maombi yake."

Hata hivyo, kauli hiyo ilisababisha mtafaruku kwa baadhi ya wasanii waliokuwepo katika jukwaa hilo, akiwamo Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini , Joseph Mbilinyi (Chadema) ambaye pia ni msanii wa muziki wa hip hop alisema kuwa wasanii nchini wananyonywa na kutumiwa kisiasa.

Alimshauri Rais Kikwete atoe tamko la wazi litakaloeleza nia na dhamira ya studio hiyo kukabidhiwa kwa Tanzania Fleva Unit, pasipo kupitia Basata.

"Hili suala limeendeshwa kisiasa zaidi, hatutaki kutumika kisiasa, ninashindwa kuelewa ni kwa sababu gani vyombo hivyo visingefikishwa Basata au vingepitia wizarani," alisema Mbilinyi.

"Katika hotuba yake bungeni, Rais Kikwete alisema kuwa kilio cha wasanii amekisikia na sasa tunaambiwa, eti amewapa wale walichokihitaji, sasa mbona hiyo studio hatuioni na tunaambiwa leo amewapa walioomba?" alihoji Sugu.

Katibu Mkuu wa Basata, Ghonche Materego alisema kuwa anaheshimu tamko la Rais Kikwete na kueleza kuwa malumbano kwa wasanii hayana tija.

"Nadhani suala ambalo lilikuwa likituchanganya kwa muda mrefu limepetiwa ufumbuzi, hivyo tamko limetolewa tayari na sidhani kama kuna haja ya kuendeleza malumbano," alisema.

Msemaji wa Kampuni ya Tanzania Fleva Unit, Said Fella ndiye aliyewakilisha umoja huo ambao ndio wanaomiliki vyombo hivyo mpaka sasa, alisema kuwa waliamua kumuengua Ruge Mutahaba katika usimamizi wa vifaa hivyo kutokana na migogoro iliyokuwa ikiendelea.

"Ni muda mrefu tangu tukabidhiwe vifaa hivyo, lakini migogoro ilikuwa haiishi, tuliamua kumuengua Ruge katika usimamizi ili tuweze kufungua studio hii na hivi sasa tumeshasajili kampuni hii hapa Basata" alisema Fela.

2 maoni

  • Maoni Sankofa 30 Machi 2011 Sankofa

    Kama walioomba ndio wanaotakiwa kupewa wapewe lakini na wengine wapewe fursa ya kuomba yao pia maana hivihivi inaonekana kama wako watakobania wenzao kama namna ya kupunguza ushindani kwenye gemu

  • Maoni Thaddeus Musembi 30 Machi 2011 Thaddeus Musembi

    Duh! Badhani rais kachemka, namna alivyoahidi, lilionekana ni suala la kitaifa, sasa liebadilika na kuwa suala binafsi (nimetoa kwa wale waloiniomba).
    Ilibidi Barasa la sanaa la taifa ndiyo wakabidhiwe au TBC kwa kuwa wao wana wataalamu. Lakini kwa namna hili suala lilivyopelekwa pelekwa unaweza ukapata jibu kwa dereva wetu hajui alama za barabarani, au anaendesha gari lisilo na deshboard, site wala wind mirror

    Natamani Mungu aendelee kuacha kuibariki Tanzania

Login to post comments

MSANII WA WIKI

Loveness

MUIGIZAJI na Mtayarishaji wa Filamu Tanzania Loveness Watson Nyota yake kwa sasa inatingisha katika tasnia ya

Soma Zaidi...

VIDEO YA MHARIRI

Off Side

Si mara ya kwanza kutazama filamu za Kanumba, lakini pia ni ukweli kwamba kila filamu anayokuja nayo

Soma Zaidi...

FILAMU ZA BONGO

Mbawa za Dino Zafunguka

MUIGIZAJI na Mtayarishaji wa filamu hapa nchini Tanzania Dennis Sweya (Dino) anatarajia kuanza kurekodi

Soma Zaidi...

WAHAPAHAPA VIDEO

You need Flash player 6+ and JavaScript enabled to view this video.