Jina la Usajili:  Neno la Siri:    Umesahau neno la siri?   |   Umesahau jina?
31 Machi 2011

Afande ampa 'shavu' Twenty Pasenti

afande

Jana usiku nyumbani kwa "Mfalme wa vina" nchini, Seleman Msindi 'Afande Sele', palikuwa hapatoshi baada ya msanii huyo kumuandalia sherehe ya kufa mtu ya kumpongeza msanii mwenzake, Abbas Hamis Kinzasa, maarufu kwa jina la 20% ambaye alifanikiwa kuvunja rekodi ya kutwaa tuzo tano kwa mpigo wakati wa utoaji tuzo za muziki za Kili Music Awards 2011 zilizofanyika wikiendi iliyopita katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.

Wakati tuzo hizo zinafanyika, 20% alikuwa Tabora kwenye moja ya shoo zake ambapo baada ya kumaliza shoo hiyo, Afande Sele alimtaka msanii huyo ashuke mjini morogoro kwa lengo la kumfanyia sherehe ya kumpongeza.

Sherehe hiyo ilifanyika kwenye nyumba ya Afande Sele iliyopo pande za Misufini mjini hapa ambapo masela kibao walifurika nyumbani kwa msanii huyo wakinywa na kula usiku kucha.

Katika hali iliyoonyesha kwamba Afande Sele alifurahia kupita kiasi kitendo cha rafiki yake kuibuka kidedea, alijisahau na kutoka kwenye hadhara akiwa amevaa ndala mguu wa kushoto wakati mguu wa kulia akiwa amevaa kiatu cha wazi kitendo kilichowavunja mbavu.

Habari na DHW

Login to post comments

MSANII WA WIKI

Loveness

MUIGIZAJI na Mtayarishaji wa Filamu Tanzania Loveness Watson Nyota yake kwa sasa inatingisha katika tasnia ya

Soma Zaidi...

VIDEO YA MHARIRI

Off Side

Si mara ya kwanza kutazama filamu za Kanumba, lakini pia ni ukweli kwamba kila filamu anayokuja nayo

Soma Zaidi...

FILAMU ZA BONGO

Mbawa za Dino Zafunguka

MUIGIZAJI na Mtayarishaji wa filamu hapa nchini Tanzania Dennis Sweya (Dino) anatarajia kuanza kurekodi

Soma Zaidi...

WAHAPAHAPA VIDEO

You need Flash player 6+ and JavaScript enabled to view this video.