Jina la Usajili:  Neno la Siri:    Umesahau neno la siri?   |   Umesahau jina?
01 Aprili 2011

Jumapili ni Usiku wa Wasafi Bills

diamond

WASANII wanaofanya vema kwa sasa kutoka familia ya ‘Wasafi’ Diamond ‘Rais wa Wasafi’, Hemed na Shetta wanatarajiwa kutumbuiza katika onyesho lililobatizwa kama ‘Usiku wa Wasafi’ utakaofanyika Aprili 6 kwenye ukumbi wa Club Bilicanas jijini Dar es Salaam.

Wakali hao, kwa sasa wako katika mazoezi makali ya kujiandaa na onyesho hilo, litakalorindima Jumapili katika probramu ya ‘Bongo Starz Nite’.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi jijini Dar es Salaam jana, mmoja ya wasanii hao, Nassib Abdul, maarufu kama Diamond, alisema usiku huo utakuwa ni zaidi ya burudani, kutokana na maandalizi wanayoyafanya.

“Kama mnavyojua mambo yetu tunayoyafanya pindi tunapopanda jukwaani, hivyo mashabiki mkae mkao wa kula siku hiyo kwa kujitokeza kwa wingi,” alisema.

Kupitia usiku huo, Diamond atashuka na nyimbo kama ‘Kamwambie’, ‘Nitarejea’, ‘Mbagala’, ‘Nalia na Mengi’, ‘Binadamu Wabaya’ na nyinginezo, huku Shetta naye akishuka na kitu kama ‘Nimechokwa’.

Naye Makamu wa Rais wa Wasafi, Hemed atashuka na vibao vyake kama ‘Si ulisema’, ‘Alcohol’ na nyinginezo, ambako kiingilio kimepangwa kuwa sh 5,000.

na Dina Ismail

Login to post comments

MSANII WA WIKI

Loveness

MUIGIZAJI na Mtayarishaji wa Filamu Tanzania Loveness Watson Nyota yake kwa sasa inatingisha katika tasnia ya

Soma Zaidi...

VIDEO YA MHARIRI

Off Side

Si mara ya kwanza kutazama filamu za Kanumba, lakini pia ni ukweli kwamba kila filamu anayokuja nayo

Soma Zaidi...

FILAMU ZA BONGO

Mbawa za Dino Zafunguka

MUIGIZAJI na Mtayarishaji wa filamu hapa nchini Tanzania Dennis Sweya (Dino) anatarajia kuanza kurekodi

Soma Zaidi...

WAHAPAHAPA VIDEO

You need Flash player 6+ and JavaScript enabled to view this video.