Jina la Usajili:  Neno la Siri:    Umesahau neno la siri?   |   Umesahau jina?
01 Aprili 2011

Msama Aiomba Radhi Shinyanga

Msama Aiomba Radhi Shinyanga

MWENYEKITI wa kamati ya maandalizi ya tamasha la muziki wa Injili la Pasaka, Alex Msama, amewaomba radhi wapenzi na mashabiki wa muziki huo wa mjini Shinyanga na vitongoji vyake kutokana na tamasha hilo kuhamishiwa jijini Mwanza.

Msama alisema jijini Dar es Salaam jana kuwa amelazimika kuomba radhi kutokana na kupata simu nyingi kutoka Shinyanga zikilalamikia hatua ya kulihamisha tamasha hilo lililokuwa lifanyike kwenye Uwanja wa Kambarage, Aprili 26.

Alisema uamuzi wa kuhamishia Uwanja wa CCM Kirumba, ni wa kamati, ingawa yeye ndiye mwenyekiti, kutokana na sababu mbalimbali.

Msama, mdau aliyechangia kwa kiasi kikubwa kukua kwa muziki wa injili nchini kupitia matamasha tangu mwaka 2000, amewataka wapenzi na mashabiki wa muziki wa injili wa Shinyanga, wawe wavumilivu.

“Nawaomba wapenzi na mashabiki wa muziki wa injili wa pale mjini Shinyanga na vitongoji vyake, watusamehe kwa kulihamisha tamasha ambalo lilikuwa lifanyike pale Aprili 26,” alisema Msama.

Alisema, huo ni uamuzi wa Kamati kutokana na sababu mbalimbali zilizo nje ya uwezo wa kamati hiyo, lakini akiwa mwenyekiti anapaswa kuomba radhi kwa niaba ya kamati yake.

Alisema, kwa vile Shinyanga wameonyesha kiu kubwa ya tamasha, kamati yake itaangalia uwezekano wa kuwapelekea matamasha mengine yajayo, kwani anaheshimu na kuthamini ukarimu wa wakazi wa Shinyanga.

Alisema onyesho la kwanza la tamasha la Pasaka, litafanyika kama ilivyopangwa Aprili 24, kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee ambako mgeni rasmi atakuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete.

Msama alisema tamasha la Pasaka litapambwa na waimbaji mahiri wakiongozwa na Rose Muhando, malkia wa nyimbo za Injili wa mwaka 2009 kwa mujibu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC1), Upendo Nkone, Bony Mwaitege, Annastazia Mukabwa, Pamela Wanderwa, Christina Shusho, Ephraim Sekeleti na Solomon Mukubwa.

Tamasha la Pasaka la mwaka huu litashirikisha waimbaji wa nyimbo za Injili kutoka nchi sita ambazo ni Kenya, Uganda, Rwanda, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Afrika Kusini na Zambia. Pia kutakuwa na kwaya mbili kutoka katika nchi hizo.

Lengo la tamasha la mwaka huu ni kuchangisha fedha kwa ajili ya watoto yatima, kuwasaidia mitaji ya biashara wajane wasiojiweza na waathirika wa mabomu yaliyotokea kambi ya JWTZ Gongo la Mboto, Dar es Salaam, Februari 16 mwaka huu.

Kiingilio katika tamasha hilo kitakuwa sh 4,000 kwa viti vya kawaida, viti maalumu (B) sh 10,000 na viti maalumu (A) sh 20,000.

Login to post comments

MSANII WA WIKI

Loveness

MUIGIZAJI na Mtayarishaji wa Filamu Tanzania Loveness Watson Nyota yake kwa sasa inatingisha katika tasnia ya

Soma Zaidi...

VIDEO YA MHARIRI

Off Side

Si mara ya kwanza kutazama filamu za Kanumba, lakini pia ni ukweli kwamba kila filamu anayokuja nayo

Soma Zaidi...

FILAMU ZA BONGO

Mbawa za Dino Zafunguka

MUIGIZAJI na Mtayarishaji wa filamu hapa nchini Tanzania Dennis Sweya (Dino) anatarajia kuanza kurekodi

Soma Zaidi...

WAHAPAHAPA VIDEO

You need Flash player 6+ and JavaScript enabled to view this video.