04 Aprili 2011

Five Star Yaibuka na - Nimeitwa Mbele Yao

Five Star Yaibuka na - Nimeitwa Mbele Yao

Wimbo Mpya wa kuwaenzi wasanii 13 wa 5STAR waliofariki kwenye ajali mbaya hivi majuzi tayari umeanza kusikika kwenye redio mbalimbali,wimbo huo uitwao MBELE YAO umetungwa na mpiga kinanda wa siku nyingi bwana THABIT ABDUL na kuimbwa na wasani mbalimbali wa muziki huo wa taarab.

Msiba huo mkubwa ambao ulitikisa tasnia ya muziki nchini naku kosakosa wasani wakubwa nchini kama HADIJA KOPA, uliwaacha mamia wakililia ndugu na jamaa zao waliowatoka gafla.

Wasanii waliyoshiriki katika kuimba wimbo huo ni mwimbaji wa kundi la TOT, Mariam Khamisi ambaye zamani alikuwa 5’Star, Omary Tego wa kundi la Coast Taarab, Hadija Kopa wa TOT, Hassan Ally na Thabith mwenyewe.

Baadhi ya waimbaji waliokuwa wamejumuishwa kuimba ambao hawakuimba ni Mzee Yusuph, kiongozi wa kundi la JAHAZI, aliyesema kuwa dini yake haimruhusu kuimbia watu waliofariki, mwingine ni Mrisho MPoto aliyekuwa safarini nje ya nchi.

Habari na Kulthum Maabad