Jina la Usajili:  Neno la Siri:    Umesahau neno la siri?   |   Umesahau jina?
04 Aprili 2011

Tumuombee Mzee Gurumo

Tumuombee Mzee Gurumo

Mke wa mwanamuziki mkongwe nchini, Muhidin Maalim Gurumo, Pili Gurumo amewataka Watanzania kumuombea mumewe ambaye amelazwa tena katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili akikabiliwa na matatizo ya presha ya kushuka.

Akizungumza na gazeti la Risasi Jumamosi, juzi (Alhamisi) Muhimbili, Pili alisema kutokana na matatizo ya mumewe anawaomba Watanzania wote, wakiwemo mashabiki wake kusali sana kwa ajili ya mumewe ili apate nafuu na kurudi nyumbani kuendelea na kazi za ujenzi wa taifa.

“Jamani, mume wangu anaumwa tena, amelazwa hapa (Muhimbili), nawaomba Watanzania wote hata wale mashabiki wake, wamuombee apone ili akalijenge taifa,” alisema Pili.

Taarifa zilizothibishwa na Afisa Uhusiano wa Muhimbili, Jezza Waziri siku ya Alhamisi zinasema kuwa, mwanamuziki huyo wa Msondo Music Band, alifikishwa hospitalini hapo Jumatano saa 2 asubuhi akiwa hajitambui.
“Ni kweli tunaye Bw. Gurumo, aliyeletwa akiwa hajitambui jana (Jumatano) saa mbili asubuhi,  ikabidi apelekwe katika chumba cha wagonjwa mahututi (ICU). Uchunguzi dhidi ya afya yake unaendelea lakini leo (Alhamisi) anaendelea vizuri ukilinganisha na wakati analetwa,” alisema Jezza.

Hii ni mara ya pili kwa mwanamuziki huyo mkongwe kulazwa hospitalini hapo. Mara ya kwanza ilikuwa ni mwanzoni mwa mwaka huu ambapo mbali na mashabiki wake, Rais Jakaya Kikwete naye alikwenda kumjulia hali.

Habari na Na Haruni Sanchawa

Login to post comments

MSANII WA WIKI

Loveness

MUIGIZAJI na Mtayarishaji wa Filamu Tanzania Loveness Watson Nyota yake kwa sasa inatingisha katika tasnia ya

Soma Zaidi...

VIDEO YA MHARIRI

Off Side

Si mara ya kwanza kutazama filamu za Kanumba, lakini pia ni ukweli kwamba kila filamu anayokuja nayo

Soma Zaidi...

FILAMU ZA BONGO

Mbawa za Dino Zafunguka

MUIGIZAJI na Mtayarishaji wa filamu hapa nchini Tanzania Dennis Sweya (Dino) anatarajia kuanza kurekodi

Soma Zaidi...

WAHAPAHAPA VIDEO

You need Flash player 6+ and JavaScript enabled to view this video.