Jina la Usajili:  Neno la Siri:    Umesahau neno la siri?   |   Umesahau jina?
05 Aprili 2011

Haleluya Collection Volume 5 kufyatuliwa Tamasha la Pasaka

Haleluya Collection Volume 5 kufyatuliwa Tamasha la Pasaka

KILELE cha tamasha la kimataifa la Pasaka litakalofanyika Aprili 24 kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee, jijini Dar es Salaam, kitakwenda pamoja na uzinduzi wa albamu mpya ya muziki wa Injili ya Haleluya Collections Vol 5.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama, itaizindua albamu hiyo iliyowashirikisha waimbaji wa ndani na nje ya nchi.Msama alisema katika albamu hiyo wameshirikishwa waimbaji kutoka nchi tatu ambazo ni Tanzania, Kenya na Uganda na waimbaji 10 huku kila mmoja akiwa na wimbo mmoja.

“Lengo la albamu hii pia ni kutambulisha waimbaji chipukizi kila mwaka na safari hii tutafanya hivyo wakati wa kilele cha Tamasha la Pasaka,” alisema Msama.

Msama aliwataja waimbaji walioshiriki kwenye albamu hiyo Vol 5 ni Rose Muhando akiwa na wimbo wake wa ‘Mungu kwetu ni kimbilio’, Geraldine Odour akiwa na wimbo wa ‘Ndoto Yangu’.

Wengine ni Bugando Choir wakiwa na wimbo wa ‘Ufisadi’, Anni Annie na wimbo wa ‘Jina la Yesu’, Jennifer Mgendi akiwa na ‘Kilio cha Uchungu’ na Josephine Thobias na wimbo wake wa ‘Fainali ya Mwanadamu’.

Wengine ni Michael Godwin na wimbo wa ‘Mapigano’, Upendo Sanga na wimbo wa ‘Kipimo’, Shengera Gospel Panorama na wimbo wa ‘Vuteri’ na Pamela Wandera na wimbo wake wa ‘Mpe Mzigo Wako’.

Albamu hiyo imeandaliwa na kusambazwa na Msama Promotions na malengo yake ni kusaidia watoto yatima na misaada kwa wajane.

Tamasha la Pasaka la mwaka huu litakuwa la aina yake kwani mgeni rasmi atakuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete.

Kwa mujibu wa Msama, tamasha hilo baada ya kufanyika jijini Dar es Salaam, siku inayoafuata Aprili 25, litalindima kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.

Aidha, Aprili 26, tamasha hilo litafanyika kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza Aprili 26 mwaka huu ambayo itakuwa Sikukuu ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Tamasha la mwaka huu malengo yake makubwa ni kuchangisha fedha kwa ajili ya kuwasomesha watoto yatima na kuwasaidia mitaji wanawake wajane.

Msama alisema, fedha nyingine zitatumika kwa ajili ya kuwasaidia waathirika wa mabomu yaliyotokea kambi ya JWTZ Gongo la Mboto jijini Dar es Salaam, Februari 16 mwaka huu.

Msama kupitia kampuni yake ya Msama Promotions, ndiye amechangia kwa kiasi kikubwa kukua kwa muziki wa injili nchini kupitia Tamsha la Pasaka, Krismasi au uzinduzi wa albamu tangu mwaka 2000.

Habari na Tanzania Daima

Login to post comments

MSANII WA WIKI

Loveness

MUIGIZAJI na Mtayarishaji wa Filamu Tanzania Loveness Watson Nyota yake kwa sasa inatingisha katika tasnia ya

Soma Zaidi...

VIDEO YA MHARIRI

Off Side

Si mara ya kwanza kutazama filamu za Kanumba, lakini pia ni ukweli kwamba kila filamu anayokuja nayo

Soma Zaidi...

FILAMU ZA BONGO

Mbawa za Dino Zafunguka

MUIGIZAJI na Mtayarishaji wa filamu hapa nchini Tanzania Dennis Sweya (Dino) anatarajia kuanza kurekodi

Soma Zaidi...

WAHAPAHAPA VIDEO

You need Flash player 6+ and JavaScript enabled to view this video.