Jina la Usajili:  Neno la Siri:    Umesahau neno la siri?   |   Umesahau jina?
05 Aprili 2011

Mwinjuma 'kimasomaso' ndani ya Vatican City

Mwinjuma 'kimasomaso' ndani ya Vatican City

BENDI ya muziki wa dansi nchini ya The African Stars ‘Twanga Pepeta’ Ijumaa ijayo inatarajiwa kufanya onyesho la utambulisho wa wasanii wake wapya waliojiunga na bendi hiyo akiwemo Muumin Mwinjuma ‘Kocha wa Dunia’.

Onyesho hilo linatarajiwa kufanyika katika ukumbi wa Vatican City Hotel ulipo Sinza, jijini Dar es Salaam ambapo mashabiki watakaojitokeza watapata fursa ya kuwashuhudia nyota hao waliojiunga hivi karibuni.

Mkurugenzi wa Afrika Kabisa Entertainment iliyoandaa onyesho hilo, Robert Ekerege, alisema jana kuwa mbali na Muumin wasanii wengine wapya ni Zena Muharami na Haji ambaye ametokea katika shindano la Bongo Star Search (BSS).

Ekerege alisema maandalizi kwa ajili ya onyesho hilo ambalo kiingilio kitakuwa sh 5,000 kwa kila mmoja yanakwenda vizuri ambapo bendi hiyo inaendelea na mazoezi makali ya kujifua kwa onyesho hilo.

Hivi karibuni Twanga Pepeta ilijiimarisha kwa kuchukua wasanii kadhaa akiwemo Khadija Mnoga ‘Kimobitel’ aliyekuwa akiimbia bendi ya Extra Bongo ‘Next Level’, pamoja na wengineo.

Hiyo inatokana na wanamuziki wake nane kunyakuliwa na bendi ya Extra Bongo iliyopo chini ya Ali Choki akiwemo mnenguaji mahiri Hassan Mussa ‘Super Nyamwela’ na wengine.

Habari na Dina Ismail

Login to post comments

MSANII WA WIKI

Loveness

MUIGIZAJI na Mtayarishaji wa Filamu Tanzania Loveness Watson Nyota yake kwa sasa inatingisha katika tasnia ya

Soma Zaidi...

VIDEO YA MHARIRI

Off Side

Si mara ya kwanza kutazama filamu za Kanumba, lakini pia ni ukweli kwamba kila filamu anayokuja nayo

Soma Zaidi...

FILAMU ZA BONGO

Mbawa za Dino Zafunguka

MUIGIZAJI na Mtayarishaji wa filamu hapa nchini Tanzania Dennis Sweya (Dino) anatarajia kuanza kurekodi

Soma Zaidi...

WAHAPAHAPA VIDEO

You need Flash player 6+ and JavaScript enabled to view this video.