Mh. Temba Print
30 Septemba 2010

Kutoka TMK, Mh. Temba na Chege wanafunga safari hadi jijini Nairobi na kupata tafu la dada anayesumbua sana anga la muziki wa Kizazi kipya kwa sasa, si mwingine, Wahu. Kwa pamoja wanakuja kupamba ukurasa wetu na wimbo wa "Weka Juu".

Jamaa wanakwambia katika juma hili sahau shida zako zote na uweke mikono juu kuonesha ishara ya kutokata tamaa.

 

Inapendeza sana jinsi wasanii wetu walivyokumbatia kwa moyo mmoja suala zima la Uafrika mashariki, wakati wanasiasa wetu bado wanacheza na makaratasi kuweka mambo sawa wao tayari wamaeshaanza kufanza mambo kwa vitendo. Kula raha na uwe na wiki njema.