AY (Ambwene Yesaya) Print
30 Septemba 2010

Ambwene Yesaya (AY) ameshanyakua tuzo za kutosha katika tasnia ya muziki, hii ikiwa ni kuanzia nchini kwake na Afrika kwa ujumla.

AY ni mmoja wa wasanii waliofanikiwa kuutoa muziki wa Afrika ya Mashariki katika mipaka yake iliyozoeleka na kuusambaza karibu Afrika yote.

 

Katika kibao chake cha "Kings and Queens" anawashirikisha mwanamuziki Amani wa nchini Kenya na mwanadada mwingine anayekwenda kwa jina la Jokate. Enjoy ze video na uwe na wiki njema.