Marlaw Print
30 Septemba 2010

Marlaw ni kifaa kingine chenye uzito wa kutosha katika sekta ya muziki wa kizazi kipya. Amekuwa kila akiingia studio na kufyatua kitu kinakuwa cha uhakika. Siku za hivi karibuni nilifanikiwa kuhudhuria harusi moja, mara baada ya utoaji zawadi MC akaamua kuwafuta watu jasho na kibao cha "Pii Pii" cha Marlaw, kufumba na kufumbua dancing floor ika imejaa si tu watoto bali na baba na mama zao nao wakigombea nafasi humohumo.

Nikaona si vibaya Marlaw akitupambia ukurasa wetu kwa kanzi nzuri aliyofanya ya kuunganisha rika tofauti katika muziki wa kizazi kipya. Kula video mdau.