Nakaaya Print
30 Septemba 2010

Huu ni mwaka wa uchaguzi. Wanasiasa kote duniani wanatambua umuhimu wa muziki katika kujikusanyia mashabiki watakaowapigia kura ili washinde. Kwa maana nyingine ni kwamba mwanamuziki akijitolea kumuunga mkono mwanasiasa fulani kuna uwezekano mkubwa kwamba wapenzi wake wakafanya hivyo pia.

Nakaya anatueleza jambo kuhusu siasa na wanasiasa katika wimbo wake wa "Mr. Politician". Sikiliza kwa makini anasema nini na anakushauri ufanye nini. Nakaya anapamba kurasa yetu kwa juma hili.