Linah Print
30 Septemba 2010

Miaka si mingi imepita ambapo ilikuwa ni nadra sana kusikia wanamuziki chipukizi wa jinsia ya kike. Leo ukifumba jicho kidogo tu mara utakapofungua utakuta wamepanga foleni ndefu, wanaibuka kila siku. Lakini ukweli unabaki kwamba si wote wanaotishia uwepo wa wasanii wakongwe.  Kati ya wachache ambao wametokea siku za karibuni na kuwafanya kuwa gumzo midomoni mwa wapenzi wa muziki ni Linah.

Linah na kibao chake cha "Atatamani" wamesumbua vituo karibu vyote vya radio na televisheni kwa kumata chati za juu za muziki. Huyu hapa Linah, anatupambia ukurasa huu kwa wiki hili.