Banana Zorro Print
19 Oktoba 2010

Banana Zorro ni mmoja wa wanamuziki wa mwanzo kabisa katika uwanja wa Bongo Flava au Muziki wa Kizazi Kipya. Banana ni mtoto wa mwanamuziki mkongwe katika tasnia ya muziki Tanzania, Mzee Ally Zorro.

Banana aliingia kwenye gemu na singo za "Anakudanganya" na "Big Boss", halafu akaunda kundi na mwenzake aliyekuwa anakwenda kwa jina la Masiga, kundi lilikuwa likijulikana kama "B love M"

Mwaka 2002, Banana akaachia albamu yake ya kwanza iliyokwenda kwa jina la "Banana", mwaka 2006 ikafatiwa na "Subira". Jamaa anasifika kama mwanamuziki 'kiraka', anachafua engo zote za muziki wa kizazi kipya, toka kwenye rhumba, mwanamuziki wa kujitegemea hadi muziki wa bendi. Utakumbuka kwamba Banana amewahi kufanya muziki na bendi kubwa ya InAfrika. Banana pia ameshirikiana na wanmuziki wengi sana kama Bushoke na Soul n Faith.

Baadhi ya nyimbo zake zilizowahi kubamba vilivyo ni Nimekuchagua Wewe, Mama Yangu, HaoHao, Nataka Niwe Nawe, Sinyota, Safari, Ninakuona, Mapenzi ya Simu, Jua Linazama, Wangu Maria, Mama Kumbena, Zoba, na zingine nyingi.

Mwaka 2010 alifanikiwa kushiriki katika tamasha kubwa kabisa la muziki katika Bara la Afrika, tamasha la Sauti za Busara.