Ferooz Print
19 Oktoba 2010

Ferooz, msanii wa muziki wa Bongo Flava, unaweza ukasema pia kuwa ni mmoja wa wasanii wa mwanzo kabisa kuweza kufaidi matunda ya kazi ya muziki hapa nchini Tanzania, alianza kuwika na kundi la Daz Nundaz mwanzoni kabisa mwa miaka ya 2000, halafu baadae akaamua kutoka kivyake na kuwika sana na kibao chake cha "Starehe". Baadae akashirikiana na Profesa Jay katika "Nikusaidiaje". Sasa anatamba zaidi na albamu ya "Sauti na Vyombo".