Adili Print
26 Oktoba 2010

Anaitwa Adili, mi huwa napenda kumwita Adili wa Chapakazi. Jamaa huwa hasemi sana ila siku akisema masikio yote yanakata kona kumsikiliza.

Hivi karibuni kashirikiana na washkaji flani na wameachia hii ngoma inayokwenda kwa jina la "Wanadata na Midosho..." Nyimbo kali, video kali, washkaji wamtulia kwenye namba, kwa nini wasikamate ukurasa huu kwa juma hili? Cheki mwenyewe halafu nambie.