MB Dogg Print
14 Machi 2011

MB Dogg ni msanii wa bongo fleva ambaye alianza shughuli zake za muziki kwa kishindo na umaarufu waake umeenea nchini Tanzani a na nchi za jirani.

Jina lake halisi ni Mbwana Mohamed na alizaliwa katika viunga vya jiji la dar mwaka 1983 na kama vijana walio wengi upenzi wake wa muziki wake umetokana na ushawishi wa muziki wa kimarekani na baadae kufuata ushawishi wa waanzilishi wa bongo fleva hapa nchini kama Mr II, Dola Soul na Kwanza Unit.

MB Dogg ambaye yuko chini ya uongozi wa Tiptop connection alitoka na wimbo wake kwa mashabiki wake mwaka 2004 uitwao Latifa, wimbo ambao ulichezwa na vituo vingi vya redio na sehemu mbalimbali Tanzania. Alichaguliwa na baadaye kushinda tuzo ya mwanamuziki wa kiume anayechipukia wa mwaka 2004/05. Nyota yake iliendelea kung'ara baada ya wimbo wake wa pili wa Si Ulinambia kupata tuzo ya wimbo bora wa mwaka 2005/06.

 

Matarajio yake ni kupata tuzo ya albamu bora ya mwaka 2006/07, kuvuka mipaka na kupata soko na mashabiki katika ukanda wa afrika mashariki. Kwa sasa anaandaa albamu yake ya pili ambayo itatoka mwaka 2007.