Matonya Print
21 Machi 2011

Seif Shaban ama kama ajulikanavyo matonya amekuwa mwanamuziki maarufu sana wa bongo fleva katika mwaka wote wa 2006. Wimbo wake wa Vailet ulimalizia mwaka ukiwa umepigwa zaidi ya nyimbo nyingine nchini.

Matonya ambaye anatokea Tanga, ni motto wa pili katika familia ya watoto wane. Alipata elimu yake ya msingi na sekondari mkoani tanga na baadaye alihamia dar ili kuweza kujiendeleza kimuziki. Upenzi wake wa muziki ulianza wakati akisoma shule pamoja na rafiki zake wane; Seif, Mark, Rama na Davie waliunda kundi lililojulikana kama Diborn Circle. Walirekodi wimbo wao wa kwanza uliokuwa ukiitwa tuko pamoja mwaka 2000. Kwa bahati mbaya kundi hili halikuendelea na hivyo kumfanya Matonya afanye kazi ya muziki kama mwanamuziki wa kujitegemea.

Uamuzi wa kujiita Matonya ulitokana na ugumu uliompata wa kuingia kwenye muziki wa bongo fleva. Matonya ni jina ombaomba maarufu jijini dar ambaye aliamriwa kurejea kwao Dodoma na  aliyekuwa mkuu wa mkoa wa dar yusuf makamba

 

Mwaka 2003 Matonya alifanikiwa kutoa albamu yake ya kwanza ambayo ilisaidiia kutangaza jina lake na kumfanya kuwa mmojawapo wa wassanii wa bongo fleva wanaoheshimika. Hata hivyo ni albamu yake ya pili ambayo ilitoka mwaka  2006 ambayo ilipata tuzo ya mwanamuziki bora wa mwaka. Katika albamu yake mpya aliwashirikisha wanamuziki kama Mr Blue, Mwana FA na Joslin.