Steve RnB Print
11 Aprili 2011

Stephen William ndiye msanii wetu wa wiki hii na yafuatayo ni mahojiano baina yangu na yeye kuhusu yeye na kile anachokifanya vema kuliko vingine nikimaanisha muziki wa kizazi kipya aka BONGO FLAVA ambaye alijiunga na Machozi Band ya Lady Jaydee na tayari amekuwa nguzo muhimu kwa bendi hiyo na hilo limetokana na umahiri wake wa kuimba nyimbo nyingi za kuiga kw ustadi zaidi.


Mimi: Mambo Steve

Steve: Poa kaka, inakuaje?

Mimi: Poa tu, mambo yanaendaje?

Steve: Shwari kama kawa.

Mimi: Sasa kaka nina maswali kadhaa hapa nahitaji kukuuliza kuhusu wewe na mahojiano haya nitayaweka katika blog yangu ili washabiki wako wapate jua umejipangaje mwaka huu.

Steve: Ok lete maswali.

1. Ni lini ulianza kufanya mziki?
Steve: Nilianza mwaka 2007 baada ya kumaliza kidato cha sita.

2.Kabla ya kushirikishwa na Mr Blu katika wimbo Tabasam ambao wewe ulisimama katika kiitiko uliwahi kutoa track yako yoyote?
Steve: Yeah nilishatoa track moja ikiitwa Nisamehe ambayo ilikuwa katika mahadhi ya Reggae.

3. Track yako Sogea karibu uliyomshirikisha Dattaz ilifanya vizuri sana na pengine ndiyo track iliyokutambulisha vema ukiondoa tambasam na iliingia katika hatua ya nominations ya tunzo za Kili za mwaka 2010 lakini haikushinda. Unafikiri una track ambayo mwaka huu itaingia katika nomination za Kili Music Awards na hatimae kushinda?
Steve: Nina imani track nilizotoa baada ya Sogea karibu ambazo ni one love na sitomwacha zina weza kunipatia tuzo mwaka huu kwani zimekubalika sana tu.

4.Umejaaliwa kuwa na mke?
Steve: Hapana sijaoa lakini ninaye rafiki wakike kwa sasa.

 

5.Una track yoyote mpya umetoa mwaka huu?
Steve: Yeah nimetoa track inayoitwa usinihukumu ambayo nimemshirikisha Maunda Zorro.

6.Washabiki wako wategemee nini mwaka huu?
Steve; Dah Mashabiki wangu wategemee mengi tu ambayo hawayajui kuhusu na watayajua kadri muda unasonga mbele.
Steve mimi nakushukuru sana na nakutakia kila la kheri katika shuhuli zako za muziki kwa leo nitaishia hapa.
Any time bro, nashukuru sana!

Mahojiano haya yalifanywa na blogu ya www.keronyingi.blogspot.com