Khadija Kopa Print
04 Juni 2011

Wiki hii ni zamu ya muimbaji mkongwe wa taarab nchini, Khadija Omar Kopa ambaye anajibu na kufafanua juu ya yale ambayo mlimuuliza.

Kwa nini za vijembe tu?
Uko juu, nakukubali sana lakini mbona unapenda kuimba nyimbo za vijembe kuliko za kawaida? Nassir Mohamed, Chamanzi Msufini, 0715 772 846.
KHADIJA ANAJIBU: Mashabiki wangu ndiyo wanapenda niimbe nyimbo za mipasho, nikiimba za kawaida wanalalamika.

Anajiaibisha
Unajiabisha, hivi kwa nini umeamua kuolewa na mwanaume mdogo kiumri? Selemani Natuku, Dar, 0718 803 204.
KHADIJA ANAJIBU: Kwangu sioni ajabu, angalia mitandao mbalimbali uwaone wasanii wakubwa wa huko nje wanavyoolewa na watoto, kuolewa siyo aibu.

Idadi ya watoto wake
Naomba uniambie zaidi ya mwanao marehemu Omary, una mtoto mwingine? Sonia, Dar, 0652 191 693.
KHADIJA ANAJIBU: Ninao wengine watatu.

Siri ya kutoihama TOT
Naomba unipe siri ya kutulia TOT bila ya kuhamahama. Sara, Dar, 0653013587
KHADIJA ANAJIBU: Nalipwa vizuri, bosi wangu Komba ananijali, niko huru na sina wasiwasi, kwa nini nihame?

Aliwahi kuolewa na Faudh
Eti ulikuwa mke wa kaka mmoja anaitwa Faudh, ulikuwa unaishi naye Mbagala? Mama Salha, Dar, 0655 660 052.
KHADIJA ANAJIBU: Ndiyo lakini tumeachana.

Huyu anamjua
Alishawahi kuwa na uhusiano na mwimbaji mwenzake Athuman Sudi. Abdi, Dar, 0719 463 000.
KHADIJA ANAJIBU: Ndiyo.

Mafanikio yake
Umedumu kwenye muziki wa taarab kwa  muda mrefu sana. Je, umepata mafanikio gani? Elia, Iringa, 0762 431 001.
KHADIJA ANAJIBU: Kiasi ninapata riziki yangu ya kila siku, watoto wanasoma na nina mahali pa kujiegesha.

Historia yake kwa ufupi
Naomba kujua historia yako kwa ufupi hadi kufikia hapa ulipo. Saimon, Dar, 0658 485 920.
KHADIJA ANAJIBU: Nimezaliwa Zanzibar mwaka 1963. Kazi ya sanaa niliianza mwaka 1990 katika Kikundi cha Culture Musical Club, mpaka sasa naendelea na sanaa.

Siri ya macho yake kuvutia
Hayo macho unatumia nini ili nami nimnunulie mke wangu maana mh! Kaunda Kaunda, Ruvuma, 0712 029 575.
KHADIJA ANAJIBU: Nimezaliwa hivyo.

Matarajio yake
Nampongeza sana kwa kazi zake. Je, matarajio yake ni yapi katika jamii? Brian, Dar, 0718 405 903.
KHADIJA ANAJIBU: Nataka nifungue ‘NGO’ yangu ili kuwasaidia watu wasio na uwezo wa kujiendeleza, wanaopenda sanaa na mambo ya kompyuta.

Mbona kimya kingi?
Mbona siku hizi upo kimya sana katika mipasho? Au ndiyo umestaafu? Kelvin David, Dar, 0713 644 447.
KHADIJA ANAJIBU: Wewe labda husikilizi redio, bado natamba mpaka nimeingia kwenye tuzo ya mwimbaji bora wa kike, naomba unipigie kura.

Ufagio
Hakuna ubishi wewe ni malkia wa mipasho. Kuna sapraizi yako siku ukija GMC Chanika. Mudy, Dar, 0717 742 546.
KHADIJA ANAJIBU: Asante sana.

Amrudie Mungu
Kutokana na umri alionao sasa, namshauri amrudie Mungu. Iddy, Tanga, 0786 279 455.
KHADIJA ANAJIBU: Mungu namjua sana na kila ninaposimama namtaja, umri siyo sababu ya kumrudia Mungu.

Macho yake vipi?
Wewe ni mlemavu wa macho au mapozi? Msomaji, 0754815665
KHADIJA ANAJIBU: Mimi siyo mlemavu, namshukuru Mungu kanipa macho mazuri yenye mvuto.

Aende mikoani
Nampenda Khadija mpaka basi, tatizo mikoani anakuja kwa nadra sana. Msomaji, 0712 548 887.
KHADIJA ANAJIBU: Asante, mikoani tunapenda kuja lakini sasa hivi gharama ni kubwa.

kundi lingine zaidi ya TOT
Dada Khadija ulishawahi kuimba kundi lingine tofauti na TOT? Rashid Musa, Newala, 0712 503 090.
KHADIJA ANAJIBU: Nimeimbia vikundi vingi sana.

Ameanza taarab lini?
Umeanza muziki wa taarabu mwaka gani? Last Voice, Mbeya, 0755 022 486.
KHADIJA ANAJIBU: Nimeanza mwaka 1990.

Aache muziki
Unaonaje ukiacha kuimba ili uitumikie ndoa yako? Jophley, Turiani, 0789 997 999.
KHADIJA ANAJIBU: Ndoa siyo ishu ya kunifanya niache kuimba, nina majukumu mengi pia siku hizi maisha ni kusaidiana.

Pongezi
Anajiheshimu kimavazi mpaka tabia, ana roho nzuri kama huna ukimuomba atakupa. Endelea na roho hiyo mama. Msomaji, 0762 465 549.
KHADIJA ANAJIBU: Asante, nashukuru.

asijaribu kujichubua
Kiukweli uko juu mama katika fani halafu una rangi nzuri sana, nakuomba usije ukajaribu kujichubua. Husnara Ajuju, Dar, 0658 906 060
KHADIJA ANAJIBU: Asante kwa ushauri wako.

Jeuri ya kujiita Malkia
Unajiita malkia wa taarabu jeuri hiyo uliipata wapi au ulipewa na nani? Msomaji, 0713300271
KHADIJA ANAJIBU: Jina la malkia nilipewa na mwandishi mmoja zamani, sijajiita mimi ila watu ndiyo wanaendelea kuniita.

Habari hii imekujia kwa hisanai kubwa ya Global Publishers, walifanya mahojiano haya na Kopa mapema mwezi wa tatu mwaka huu