Loveness Print
10 Julai 2011

MUIGIZAJI na Mtayarishaji wa Filamu Tanzania Loveness Watson Nyota yake kwa sasa inatingisha katika tasnia ya filamu hii Binti huyu pamoja na kuwa mtayarishaji lakini pia ni mtunzi wa filamu, msambazaji na muigizaji mwenye kipaji cha hali ya juu na hilo unalipata katika filamu yake ya Impossible Promise aliyoigiza kwa kiwango cha juu na kuonyesha uwezo wake alio nao.

Love anamiliki kampuni yake ambayo inajulikana kwa jina la Enea Production yenye maskani yake Jijini Dar es Salaam, kampuni hii ni moja kati ya kampuni zinazosaidia wasanii wapya wenye vipaji ambao hawapati nafasi za kiuigiza na Masuper Star, lakini kwa kupitia kampuni ya mwanadada huyu wanapata nafasi ya kuonyesha vipaji vyao katika filamu zinazoandaliwa na kampuni ya Enea Porduction.

“Pamoja na kutengeneza filamu lakini pia nina wajibu wa kutambulisha vipaji vya Wasanii wengine ambao pamoja na vipaji vya ukweli lakini wameshindwa kushirikishwa katika filamu na nyota wa filamu wa hapa Nyumbani hata kama wanauwezo mkubwa, na wakati mwingine unakuta wasanii ni wengi si rahisi wote kucheza katika filamu moja, pia ni vigumu kuonyesha vipaji vyao” Anasema Love.

Msanii huyu hadi ameshiriki filamu kama vile Impossible Promise, Continues love , uzio , Fake love, Sheria Mkononi, Penzi la utata, pamoja na filamu nyingine ambazo bado zipo jikoni zikisubiri kuingia sokoni kuanzia sasa.