Juma Nature na Mitindo Huru Print
28 Septemba 2010

Juma Nature ni jina kubwa katika muziki wa Kizazi Kipya au Bongo Flava. Nature pia ni mmoja wa wanamuziki wa mwanzo kabisa kuanza kufaidi matunda ya kazi ya muziki. Unaweza ukasema kwamba yeye ni mmoja wa wasanii wa mwanzo kujihakikishia soko la kazi yake.

Kila mara Nature anapofanya onesho la muziki wake, kwa mfano, amekuwa kiuza tiketi zipatazo zote kama si zote. Ni mmoja wasanii wachache sana ambaye amefanikiwa kuujaza ukumbi maarufu wa maonesho, Dimond Jubilee Hall", si mara moja bali mara zaidi ya moja. Utakumbuka kwa mfano miaka ile alipozindua albamu yake iliyokwenda kwa jina la "Ugali", ukumbiani hapakuwa na pakukanyaga.

Lakini watu wengi hukosea kwa kudhani kwamba umaarufu wa Juma Nature ni kitu kilichokuja kwake kwa bahati, ukweli ni kwamba Nature ameujenga umaarufu wake tangu nyumbani kwao, mtaani kwao, wilayani kwao, na hatimae jijini anapoishi na nchi yote ya Tanzania.

Katika video hii unaweza kujionea jinsi alivyo na wafuasi wengi huko wilayani kwake Temeke. Nature amekuwa na utaratibu wa kwenda katika fukwe ya bahari ya Hindi iliyoko Kurasini mara kadhaa kufanya mazoezi ya kughani mashairi yake au muziki wake. Hapa anafanya kitu tunaita Mtindo Huru au kwa wazungu wanaita Free Style. Tazama kiwango...