Wahapahapa Ndani ya Runway Print
28 Septemba 2010

Bendi ya Wahapahapa inatumbuiza kila Alhamisi katika ukumbi wa Runway pale Shopper's Plaza, kiingilio huwa ni mguu wako na upenzi wako kwa muziki wa nyumbani. Wahapahapa inapiga muziki aina ya TanzRock ambao una vionjo vya ngoma mbalimbali za asili za wabongo wakichanganya na mirindimo ya kimagharibi na ile ya Kimashariki pia.

Ukija kwenye shoo zao utacheza kuanzia mduara, mdundiko, na hata mchiriku. Kinachotia ladha ni vile wana bendi hawa wamaefanikiwa kuuchukua muziki huu na kuuboresha kufikia kiwango cha kimataifa. Njoo Runway kila Alhamisi, ukija mara moja katu hutoacha kutia maguu.

Lamba video la Wahapahapa Band.