Mwisho Wake Lini? Print
28 Septemba 2010

Tangu nilipomsikia Afande Sele kwa mara ya kwanza kabisa nilifahamu kuwa muziki hatimae umepata wa kuutumikia. Siku zote huyu mshkaji amekuwa na busara zilizomshinda  umri na umbo lake. Katika wimbo huu wa "Mwisho wake Lini?", mkali mwingine, "Tycoon", anamshirikisha mkali wa rhyms na kwa mara ya kwanza kabisa tangu mwaka huu uanze tunapata kibao ambacho kinatukumbusha sisi ni akina nani, tumetoka wapi, tuko wapi, na wapi tunakwenda.

Tazama video hii halafu utaelewa nasema nini.