Mbawa za Dino Zafunguka Print
25 Julai 2011

MUIGIZAJI na Mtayarishaji wa filamu hapa nchini Tanzania Dennis Sweya (Dino) anatarajia kuanza kurekodi filamu katika nchini mbili tofauti yaani Tanzania pamoja na nchi ya Namibia, filamu hii ambayo inatarajia kuteka hisia za watu ni hadithi ya kipekee kabisa kwani ni hadithi inayohusu Marafiki wawili walioshibana kuanzia shule ya Msingi hadi wanapofika elimu ya juu lakini baadae yanatokea mauaji makubwa, Je sababu ni nini?

Mtunzi wa filamu hii ambaye ni Dino mwenyewe anasema kuwa ni mapema sana kueleza kisa hiki kwa sasa lakini jambo la kwanza katika matayarisho limekamilika na anashughulikia mipango midogo midogo kwani filamu hii inaanza kurekodiwa nchini Namibia kisha kumalizikia nyumbani Tanzania.

“Hadithi ni nzuri lakini tatizo lilikuwa ni jinsi gani ya kuweza kuwakilisha katika uhalisia, ni lazima kusafiri kutoka nchi moja kwenda nchi nyingine, baada ya kukubaliana na mwenzangu Mwisho na kuchagua nchi za kuichezea filamu hii, tayari Mwisho amesafiri kwenda Nchini Namibia ambako tunatarajia kuanza kurekodi hivi punde, na mimi nipo hapa kwa ajili ya kukamilisha mambo fulani kisha naondoka” Anasema Dino.

Katika filamu hii ambayo inatarajia kuwashirikisha wasanii wa Namibia na Tanzania, kutoka Tanzania Wasanii Nyota ni pamoja na mke wa Mwisho Marry ambaye alikuwa mshiriki wa Big Brother Africa All Stars, Mwisho Mwampamba, Dennis Sweya (Dino) ni filamu inayokusudia kufungua milango kwa Watayarishaji wengine kufuata hadithi za filamu zao kama zinawahitaji wasafiri basi ni muhimu kufanya hivyo. HONGERA DINO KWA KUANZA.